Mzozo kuhusu bajeti ya EU

Imebadilishwa: 23 Novemba, 2012 - Saa 10:28 GMT

Viongozi wa Ufaransa na Ujerumani wamesema kuwa wana shaka ikiwa makubaliano yaliyofikiwa kuhusu bajeti ijayo ya muungano wa ulaya katika mkutano wa EU unaoendelea.

Rais wa ufaransa Francois Holland na Chancella wa Ujeruamani, Angela Merkel walisema hayo baada ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano huo ambao ulifanyika saa tatu baada ya muda uliotarajiwa kutokana na tofauti zilizokuwepo kuhusu mipango ya bajeti.

Mazungumzo hayo yameahairishwa hadi baadaye alasiri hivi leo.

Mapema rais wa baraza la muungano huo wa ulaya Herman Van Rompuy, alisambaza mapendekezo yaliyofanyiwa mabadiliko ya bajeti mpya na kusema kuwa anaamini kutakuwa na masikizano.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.