Wakamatwa kwa pesa haramu Bolivia

Imebadilishwa: 28 Novemba, 2012 - Saa 08:52 GMT

Waziri wa mambo ya ndani wa Bolivia, Carlos Romero, amesema kuwa maafisa kadhaa wa serikali wametiwa mbaroni kwa kujaribu kupokea pesa kutoka kwa mfanyibiashara mmoja kutoka Marekani ambaye anahudumia kifungo cha jela nchini humo.

Wale waliokamatwa ni pamoja na mkurugenzi wa maswala ya kisheria katika wizara ya mambo ya ndani Fernando Rivera.

Mfanyibiashara huyo wa mjini New York , Jacob Ostreicher, alikamatwa mwaka uliopita kwa kosa la kuhamisha pesa nyingi bila kibali baada ya kuekeza dola milioni ishirini na tano katika biashara ya uzalishaji wa mpunga nchini Bolivia.

Amesema mashtaka dhidi yake ni hila ya kutaka kumpokonya pesa zake.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.