Watu wauawa kwenye milipuko Damascus

Imebadilishwa: 28 Novemba, 2012 - Saa 11:28 GMT

Shirika la habari linalomilikiwa na serikali ya Syria SANA limeripoti kuwa kumetokea milipuko miwili katika mji wa Jarmana,kilomita kumi kutoka mji mkuu wa Damascus, na kuwauwa watu kadhaa na kuwajeruhi wengine.

Shirika hilo linasema magaidi ndio waliohusika katika mashambulio hayo. Kundi la upinzani la Syrian Observatory for Human Rights linasema milipuko hiyo ilisababishwa na mabomu yaliyotegwa kwenye magari mawili.

Mwandishi wa BBC mjini Jarmana anasema kulikuwa na mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi katika mji huo mapema hivi leo Jumatano.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.