Marufuku kuwinda wanyamapori Botswana 2014

Imebadilishwa: 30 Novemba, 2012 - Saa 09:02 GMT

Botswana itapiga marufuku uwindaji halali wa kibiashara wa wanyamapori ifikapo Januari 2014 kwa sababu ya wasiwasi unaozidi kukua kuhusu kushuka kwa kasi kwa idadi ya wanyamapori, duru za dola zimesema.

"Kuuwawa kwa wanyamapori kwa ajili ya kujistarehesha tu au kumiliki nyara haiendi sambamba na nia yetu ya kutunza mazingira nchini," wizara ya mazingira ilisema.

Marufuku hii inaweza ikazua ubishi kwa sababu ni jamii nyingi ambazo hutegemea mawindo kama riziki yao.

Takriban thuluthi moja ya ndovu wote duniani wanapatikana nchini Botswana, na makisio ya hivi majuzi yanakisia kuwa idadi hiyo ni takriban ndovu 130,000.

Watunza mazingira wana wasiwasi kuhusu kumomonyoka kwa kingo za mito kunakofanywa na wanyama hao mbugani, alisema Letlhogile Lucas, mwandishi habari wa BBC huko mji mkuu wa Gaborone.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.