Kandanda: Senegal yapigwa faini

Imebadilishwa: 30 Novemba, 2012 - Saa 11:03 GMT

Shirikisho la Soka Barani Afrika limeipiga marufuku Senegal isitumie uwanja wa Leopold Sedar Senghor, Dakar, kwa michuano ya kimataifa kwa kipindi cha mwaka mmoja kama adhabu ya vurugu iliyotokea wakati wa mechi mnamo mwezi Oktoba.

Shirikisho la Kandanda la Senegal pia lilipigwa faini ya dola za Kimarekani 100,000 kwa vurugu zilizofanywa na makundi ya mashabiki baada ya mchuano wa mchujo wa kuwania Kombe la Afrika dhidi ya Ivory Coast.

Sasa itabidi timu hiyo ya Teranga Lions itafute kiwanja kingine kwa ajili ya michuano ya mchujo itakayofanyika mwaka ujao ya Kombe la Dunia 2014. Watacheza na Angola, na Uganda.

Mnamo 2007 Togo iliadhibiwa baada ya mashabiki wao kuzua fujo baada ya kutupwa nje ya mchuano wa Kombe la Afrika la 2008 na wageni Mali.

Iliibidi Togo icheze michuano mitatu iliyofuatia katika kiwanja ambacho kilikuwa hakihusishwi na upande wowote, na ikapigwa marufuku kucheza katika kiwanja cha kimataifa kwa muda wa miezi sita.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.