Mawasiliano yakatizwa Syria

Imebadilishwa: 30 Novemba, 2012 - Saa 06:52 GMT

Syria imepata pigo kubwa sana la mawasiliano tangu ghasia dhidi ya Rais Bashar al-Assad kuanza miezi 20 iliyopita.

Huduma za mtandao na simu za rununu zilikatika katika mji mkuu wa Damscus pamoja na maeneo ya katikati mwa Syria.

Kumekuwa na mapigano zaidi huko Damascus na karibu na uwanja wa ndege, kati ya vikosi vya serikali na waasi.

Kulikuwa na safari moja tu ya ndege iliyofanikiwa Alhamisi.

Serikali inasema hali hiyo ilisababishwa na waasi, lakini duru zinaeleza kuwa ni serikali ndiyo iliyokatiza mfumo wa mawasiliano ili kuzuia mawasilaino kati ya wapiganaji waasi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.