Ghasia kuhusu bendera Belfast

Imebadilishwa: 4 Disemba, 2012 - Saa 09:20 GMT

Mamia ya watu wameshiriki katika maandamano yaliokuwa na vurugu kaskazini mwa Ireland baada ya madiwani mjini Belfast, kupiga kura kuunga mkono kuiondoa bendera ya muungano kutoka manispaa ya mji huo, kwa karibu ya mwaka mmoja.

Maafisa takriban watano wa polisi walijeruhiwa wakati waandamanaji, wanaotaka kuwa sehemu ya Uingereza, walipowarushia mawe na chupa.

Kanisa moja katoliki lilishambuliwa baada ya jaribio lililotibuka la kuivamia manispaa ya mji huo.

Bendera hiyo ya muungano imekuwa ikipeperuka juu ya Manispaa hiyo tangu ifunguliwezaidi ya karne moja iliyopita.

Katika agizo hilo, bendera hiyo itapeperushwa kwa siku kumi na saba pekee kwa mwaka.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.