Wahudumu wa afya wagoma Italia

Imebadilishwa: 4 Disemba, 2012 - Saa 09:04 GMT

Wahudumu wa afya mjini Madrid nchini Uhispania wanafanya mgomo wa siku mbili dhidi ya mpango wa serikali kubinafsisha sekta ya afya.

Hospitali na kliniki zinatarajiwa kutoa huduma kidogo wakati wa mgomo huo. Serikali ya jimbo hilo inasema ubinafsishaji utasaidia kuiweka sawa bajeti yake, katika wakati ambapo hatua kali za kubana matumizi zimeidhinishwa nchini.

Wafanyakazi elfu sabini na tano wa afya wanatarajiwa kushiriki katika mgomo huo na vyama kadhaa vya wafanyakazi vimeitisha mgomo uendelee kwa muda usiojulikana.

Katika maandamano ya awali, wafanyakazi walishikana mikono na kubeba mabango yaliokuwa na ujumbe 'ikumbatie hospitali yako'.

Wafuasi wao walijiunga nao wakiwemo wagonjwa, waliojitokeza wakiwa wamevalia magauni ya hospitali. Wanagoma dhidi ya mpango wa serikali ya jimbo hilo, kubinafsisha hospitali sita kuu na kliniki ishirini na saba katika mji mkuu huo.

Katika mpango huo, madaktari na wauguzi wataajiriwa kutoka mashirika ya kibinafsi. Serikali ya jimbo hilo inayokabiliwa na ukosefu wa fedha, inasema hili litasaidia kuhifadhi fedha.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.