Berlusconi heunda akarejea mamlakani

Imebadilishwa: 7 Disemba, 2012 - Saa 09:29 GMT

Chama cha aliyekuwa waziri Mkuu wa Italia Silvio Berlusconi kinasema kuwa mwanasiasa huyo ameashiria kuwa huenda akarejea mamlakani.

Chama cha People of Freedom, kilichobuniwa na Bwana Berlusconi kinasema kimefutilia mbali mipango ya kuandaa kongamano la kumchagua kiongozi wake kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Kilisema hii ni baada ya Berlusconi kuwaelezea maafisa wa chama hicho kuwa atawaongoza katika uchaguzi huo.

Lakini hadi kufikia sasa hakuna taarifa ya moja kwa moja kutoka kwa Bwana Berlusconi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.