6 wauawa katika kituo cha polisi Pakistan

Imebadilishwa: 10 Disemba, 2012 - Saa 12:27 GMT

Polisi wa Kaskazini Magharibi mwa Pakistan wanasema kuwa wati sita wameuawa katika shambulio lililofanyiwa katika kituo kimoja cha polisi.

Msemaji wa polisi alisema kuwa watu wanne wa kujitolea mhanga walitumia gruneti na bunduki za rashasha kuvamia kituo cha polisi katika mji wa Bannu. Shambulio hilo lilizua ufyatulianaji wa risasi ambao ulidumu kwa zaidi ya saa moja.

Maafisa watatu wa polisi na raia watatu waliuawa katika shambulio hilo. Wavamizi hao walitumia msikiti uliokuwa karibu nao kama ngao kijikinga kutoka na risasi za polisi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.