Watangazaji wa redio Australia waomba radhi

Imebadilishwa: 10 Disemba, 2012 - Saa 10:13 GMT

Watangazaji wawili wa Australia waliopiga simu ghushi hospitalini alipokuwa amelazwa mkewe Prince William, aliye mja mzito, wanasema wamehuzunishwa sana na kifo cha muuguzi aliyepokea simu hiyo.

Jacintha Saldanha alikutwa kafariki siku tatu baada ya kupokea simu iliyokuwa inaulizia kuhusu hali ya Duchess wa Cambridge, aliyekuwa hospitalini akiuguzwa ugonjwa unaohusika na mimba yake.

Watangazaji hao walimhadaa muuguzi huyo kwa kujifanya kuwa walikuwa Malkia na Prince Charles.

Rhys Holleran, anayemiliki kituo hicho kilichohusika, alisema kifo cha Bi Saldanha kilikuwa cha kusikitisha, lakini hakingeweza kutabirika.

Katika mahojiano na kituo cha redio cha 3AW, mjini Melbourne, Holleran alisema wafanyikazi wake walijaribu mara kadhaa kuwasiliana na Bi Saldhana na muuguzi mwingine katika Hospitali hiyo ya King George the 7th mjini London ili kujaribu kupata idhini yao kutangaza simu hiyo ya mzaha.

Msemaji wa hospitali hiyo, hata hivyo, alisema hakuwa na lolote la kusema kuhusu madai ya Bwana Halloran.

Wataalamu wa sheria nchini Australia wanasema iwapo kituo hicho hakikuwaelezea wauguzi hao kuwa walikuwa wakirekodiwa au kupata idhini yao kutangaza mahojiano hayo, huenda basi walivunja shera kadhaa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.