Muungano wa Ulaya kukabidhiwa tuzo la Nobel

Imebadilishwa: 10 Disemba, 2012 - Saa 09:39 GMT

Muungano wa Nchi za Ulaya utakabidhiwa tuzo la amani la Nobel baadaye leo nchini Norway.

Kamati ya Nobel, yenye makao yake mjini Oslo, ilisema Muungano wa Nchi za Ulaya ulipewa tuzo hiyo kwa sababu ya jukumu lake la kuliunganisha bara Uropa baada ya Vita vya Dunia vya Pili.

Lakini wakosoaji wanasema tuzo hiyo haifai, hususan wakati huu ambapo muungano huo unapokabiliwa na mzozo wa sarafu ya euro, uliofichua tofauti zilizopo kati ya wanachama wa muungano huo.

Takriban viongozi 20 wa muungano huo, akiwemo Chansela wa Ujerumani Angela Merkel, na rais wa Ufaransa Francois Hollande, watahudhuria sherehe hiyo mjini Oslo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.