Waasi wa Syria wateka kambi ya jeshi

Imebadilishwa: 10 Disemba, 2012 - Saa 12:52 GMT

Waasi wanaopambana na jeshi la Serikali nchini Syria, wamesemekana kutwaa sehemu kubwa ya kambi ya jeshi la serikali karibu na mji wa Aleppo.

Hili ndio tukio la hivi karibuni la shambulizi dhidi ya majeshi ya serikali.

Kambi hiyo ambayo ni kubwa katika eneo la Sheikh Suleiman, ilikuwa kambi kubwa pekee au maslahi makubwa zaidi ya serikali yaliyokuwa yamesalia Kusini mwa mji huo.

Waasi wangali wanadhibiti nusu ya mji huo, licha ya hatua za serikali kujaribu kuwaondoa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.