Maswali kuhusu simu

Maswali yaulizwayo mara kwa mara kuhusu upakuaji wa sauti na video kupitia simu za mkononi

AV maana yake nini?

AV ina maana ya huduma ya sauti na video, na kwa muktadha huu inahusu maudhui yanayopatika katika sauti na video. Je ninawezaje kuangalia au kusikiliza AV kwenye simu ya mkononi? Kuangalia video zetu au kusikiliza sauti unahitaji kuwa na kifaa kinachostahili. Pia utahitaji kuwezesha kadi ya SIM kuweza kupokea data kupitia mfumo wa GPRS na WAP. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na kampuni yako ya simu.

Fomati gani zinapatikana katika bbcswahili.com?

Kupitia tovuti yetu ya mobile tunatoa: - 3gp - mp3 Kupitia tovuti ya kawaida tunatumia: - RealMedia - Windows Media

Ni gharama kiasi gani?

BBC haitozi kiasi chochote cha fedha kwa huduma ya habari kwa simu. Kampuni yako ya simu inaweza kutoza kwa kutumia mfumo wake. Kampuni za simu zinaweza kutoza kwa muda uliotumia kurambaza au kwa data zinazopakuliwa. Endapo hauna uhakika itakugharimu kiasi gani, kabla ya kutumia wasiliana na kampuni yako ya simu.

Inachukua muda gani kupakua?

Swala hili hutegemea na kasi ya wavuti unayounganishia. Katika hali ya kawaida, kipogo hupakuliwa kwa muda wa kati ya dakika moja au mbili.

Ninawezaje kusikiliza kipogo cha sauti?

Chagua faili unalotaka na mara baada ya kupakua, faili litaanza kujicheza lenyewe. Endapo halianzi kucheza, rambaza folda ulikohifadhi na jaribu kuanzisha kutoka huko. Kumbuka kuwa endapo umehifadhi sms nyingi, picha au video na kumbukumbu imejaa,unaweza kutakiwa kufuta baadhi ya mafaili kuongezeka.

Ninawezaje kutazama video?

Fuata maelekezo hapo juu sawa na kusikiliza kipogo cha sauti.

Je inawezekana kuimarisha ubora wa sauti?

Kwa kawaida ubora wa sauti kwenye simu ya mkononi kupitia speaker za ndani ni mdogo, kwa hiyo tunashauru utumie headphone.

Je ninaweza kutumiwa kiunganishi cha ukurasa wa mwanzo wa BBC World Service kupitia sms?

Hapana, hiyo haiwezekani.

Je ninaweza kusikiliza matangazo ya BBC wakati yakirushwa hewani kupitia tovuti ya simu?

Kwa sasa hatutoi huduma yoyote ya matangazo ya AV moja kwa moja kupitia simu za mkononi.

Je ninaweza kupata BBC iPlayer kwenye simu?

Kwa maelezo zaidi kuhusu vifaa gani vinaweza kutumia BBC iPlayer na vipi vinaweza kupakua vipindi kutazama moja kwa moja, tafadhali tembelea:

http://iplayerhelp.external.bbc.co.uk/help/mobile/mobile_phone