Masharti ya kutumia World Cup Team Talk

World Cup Team Talk ni shughuli itakayoshirikisha lugha mbali mbali kwa kutumia huduma ya tafsiri kwa kompyuta kutoka Google. Tunataka kuona ni jinsi gani tafsiri ya kufanywa kwa mashine inaweza kupangua vizingiti vya lugha.

Kwa kushiriki katika majaribio haya unakubaliana na masharti na kanuni zifuatazo:

  • Tafsiri zilizofanywa na mashine zitakazoonekana katika lugha nyingin huenda zisiwasilishe maoni yako halisi;
  • BBC inaweza kufuta maoni ya mtumiaji yoyote ambayo yataonekana kukiuka maadili au yanachafua sifa ya mtu au nchi au timu.

Maoni yatakuwa yakisimamiwa na kukaguliwa kikamilifu. Tunakusudia kujumuisha maoni mengi kadri iwezekanavyo, kwa hiyo tafadhali andika maoni pasipo meneno mengi.

Tafadhali epukana na matumizi ya kuandika kwa kifupi au misemo, haitaweza kutafsiriwa vizuri. Kwa kufanya hivyo utawezesha mazungumzo kufanyika vyema, kwa usalama na katika hali inayokubalika kwa wote.

Tutatumia kanuni na sheria za BBC (bofya hapa) kama vigezo vya kuchapisha au kutochapisha maoni yako. Endapo utahisi maoni fulani si sahihi, tufahamishe kwa kutumia kiunganishi cha "lalamikia maoni haya".

Tafadhali tueleze kanuni gani zimekiukwa na wasimamizi wetu wataamua endapo waondoe maoni yako au la. Kanuni za tovuti nyingine za BBC na masharti ya faragha pia zinahusika.