Mazungumzo ya BBC katika Kombe la Dunia

Soka ni lugha halisi za dunia. Kokote uendako, mashabiki wa soka hupenda kuzungumzia timu zao na wachezaji nyota wa kimataifa.

Kama sehemu ya matangazo ya BBC kuhusu Kombe la Dunia, tungependa kuwakutanisha mashabiki bila kujali lugha wanayozungumza. World Cup Team Talk, inatoa fursa kupiga hatua moja zaidi, kuwa na mazungumzo ya kimataifa kwa lugha mbali mbali.

Baadhi ya Idhaa zetu kubwa zinashirikiana kufanya mazungumzo wakati wa mechi ya ufunguzi na mechi ya fainali ya Kombe la Dunia. Mazungumzo kutoka lugha moja hadi nyingine yatafanyika kwa kutumia mfumo wa kompyuta. Maoni yatakayoandikwa katika lugha moja yataonekana katika lugha nyingine 10.

Mpango huu unafuatia majaribio ya kilele cha Superpower, ambao uliwakutanisha watu kutoka dunia nzima kupitia tafsiri ya kompyuta na kuweka kando vizuizi vya lugha Wakati huu tumeongeza uwezekano wa kujibu ujumbe wako na kufahamu idhaa husika imependezwa na maoni gani.

Msisitizo wetu si kiwango au ubora wa tafsiri, lakini ni kuwakutanisha mashabiki kutoka kote duniani kubadilishana mawazo bila kujali lugha wanazozungumza. Lengo letu ni kuwezesha watu kuona, kusikia na kusoma kile wanachojadili mashabiki wa soka kutoka sehemu nyingine duniani, na kuweza kufuatilia mazungumzo hayo.

Huenda mfumo usitoe tafsiri sahisi. Huenda tafsiri ikaonekana kituko. Itabidi tusimamishe mazungumzo na tuanze upya – kama inavyokuwa kwa mazungumzo mengine.

Hata hivyo utalazimika kuheshimu kanuni zetu ili kuepusha kuwaudhi au kuwachafulia sifa watu wengine.

Mfumo wa tafsiri kupitia tovuti (automatic translate) tunaotumia ni Google translate.

Kuna huduma nyingine za kufanya tafsiri kwenye tovuti. Baadhi ya zilizo maarufu zaidi ni: Yahoo's Babel Fish Bing Translator.

Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu nyenzo hizi za tafsiri kwa kufungua viunganishi vifuatavyo:-

Yahoo's Babel Fish

Bing Translator

Tunashukuru kwa ushiriki wako.