Inagharimu kiasi gani kutumia huduma za BBC kwa simu?

BBC haitozi kiasi chochote cha fedha kwa huduma ya habari kwa simu. Kampuni yako ya simu inaweza kutoza kwa kutumia mfumo wake.

Kampuni za simu zinaweza kutoza kwa muda uliotumia kurambaza au kwa data zinazopakuliwa.

Kwa mfano, endapo kampuni ya simu anatoza dola mbili kwa MegaByte ya data iliyopakuliwa, kurasa tatu za habari za BBC zinaweza kugharimu dola 0.20. Tafadhali wasiliana na kampuni yako kupata maelezo ya gharama.

Hata hivyo, kuna njia kadhaa unazoweza kutumia kupunguza za kurambaza wavuti kupitia simu yako:

Nunua

Kujiunga na ada ya jumla ya kila mwezi itakusaidia badala ya kulipa kwa gharama unazotumia, hasa kama ni mtumiaji wa sauti, video na mengineyo Wasiliana na kampuni yako ya simu kwa maelezo zaidi.

Tumia wi-fi

Idadi kubwa ya simu zinazouzwa sasa zinakuwa na teknolojia ya wi-fi. Unaweza kupunguza gharama za simu kwa njia hii, kupitia huduma ya broadband ya nyumbani au eneo lolote lenye wi-fi. Endapo hauna uhakika kama simu yako ina wi-fi, wasiliana na kampuni iliyounda simu yako au kampuni ya simu.

Tumia bluetooth

Baadhi ya vipogo vilivyopo katika BBC Mobile havijawekewa haki miliki na unaweza kutuma katika simu nyingine kwa njia ya Bluetooth ukawapatia pia marafiki zako.