Magazine

Msafishaji madirisha aliyeanguka kutoka ghorofa na kuishi

Alcides Moreno
Image caption Moreno na kaka yake mdogo Edgar walikuwa wamepanga kusafisha madirisha ya jengo la ghorofa 47-la kifahari la Solow Tower lililoko Manhattan mjini New York

Ni nusu tu ya watu wanaoanguka kutoka magorofa ya tatu wanaoweza kuishi. Kuanguka kutoka ghorofa la 10 kuishi ni jambo ambalo haliwezekani. Hii li hadithi ya msafishaji madirisha aliyeanguka kutoka ghorofa la 47-la moja ya majengo marefu zaidi mjini New York .

"Kusema ukweli ninapenda kuona madirisha yakiwa safi," Alcides Moreno anasema.

"Nilipenda maji na sabuni, jinsi unavyosukuma na kukamua maji kwenye madirisha .

"Tulikuwa tunaanzia juu na kusafisha hadi chini,niliipenda sana kazi yangu."

Moreno na kaka yake mdogo Edgar walikuwa wamepanga kusafisha madirisha ya jengo la ghorofa 47-la kifahari la Solow Tower liliko Manhattan upande wa juu wa mashariki tarehe 7 Disemba 2007.

Walipanda kambarau hadi kwenye ghorofa la juu , wakati wa msimu wa barafu.

Image copyright Google
Image caption Jengo la Solow Tower mwezi Mei 2016

Lakini muda mfupi baadae, mkasa ukatokea . walipopanda umbali wa futi 16 , waya wa uzio wa kuoshea madirisha "ulikatika ", kwa mujibu ripoti ya idara ya Marekani ya ajali kazini.

" Upande wa kushoto wa waya ndio uliokatika kwanza. Hii ilikuwa sehemu alipokuwa kaka yangu. Kaka yangu akaanguka , hadi chini", Alcides Moreno anasema.

Edgar alianguka kutika futi 472, na kuangukia kwenye njia nyembamba. Upande wa Alcides Moreno ulilegea muda mfupi baadae nae pia akaanza kuseleleka kuelea ardhini.

Mtaani wazima moto na madaktari wa uokoaji walibaini tukio la kutisha.

Edgar Moreno alikuwa amefika ardhini kwenye uzio wa mbao, mwili wake ulikuwa umeumia na hakuweza kusaidiwa.

Alcides Moreno alipatikana akiwa anaelea kwenye waya wa chuma uliosukwa.

Alikuwa bado anapumua , alisemakana kuwa alijitahidi kusimama.

Zimamoto walikumbuka jinsi walivyoanza kumhamishia katika katika ambilansi "kama yai linaloweza kupasuka", wakifahamu kuwa wakikosea tu kidogo katika kumbeba wanaweza kumuua.

Image copyright NYC Fire Department
Image caption Alcides Moreno (kati kati) alikutana na wahudumu wa idara ya zimamoto waliomuokoa mwaka 2008

Alcides Moreno alikimbizwa kwenye hospitali ya karibu na kuwekwa kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi.

Alikuwa na majeraha kwenye ubongo , uti wa mgongo, kifuani, na sehemu ya tumbo na alivunjika mbavu, mkono wa kulia na miguu yake miwili.

Alifanyiwa upasuaji kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuwekewa mrija wa kusaidia kupunguza kuvimba kwa ubongo wake.

Aliongezewa vijifuko 24 vya damu.

Alcides Moreno aligutuka karibu wiki tatu baadae, katika siku ya Krismasi 2007, na wakati huo alikuwepo mkewe , Rosario, kando ya kitanda chake cha hospitali.

" Nilikuwa naona maluweluwe,"anasema .

Hakukumbuka nini kilichotokea hata kuhusu namna alivyoanguka.

Je alifahamu kilichotokea kwa kaka yake?

"Nilifahamu kuwa lazima angekuwa amekufa kwasababu nilipofungua macho nilijiona mimi tu na mke wakee," alisema.

Image copyright Google
Image caption Jengo la Solow Tower mwezi Mei 2016

Makaka hao wawili wana asili ya Ecuador, na waliwasili Marekani miaka ya 1990 kutafuta kazi.

Image caption Edgar Moreno (kushoto) ana Alcides

" Kumpoteza ilikuwa na pigo kubwa kwangu," anaeleza Alcides Moreno.

"Edgar aliishi nami New Jersey, na tulishirikiana mambo mengi. Alifanya kazi nami na alikufa akifanya kazi nami .

"Niliishi kwa maisha ya huzuni kwa miaka miaka karibu mitatu .Huo ndio muda niliochukua kupona na kukubali kifo chake.

Ilikuwa ni kama kumkosa mwanangu, kwasababu alikuwa mdogo kwangu ."

Alcides Moreno alipewa malipo ya fidia na familia yake ilihamia Phoenix, Arizona. Anasema hali ya hewa ya joto huko ni nzuri kwa mifupa yake.