Umoja wa Mataifa kuijadili Korea Kaskazini

Mkutano wa Umoja wa Mataifa
Maelezo ya picha,

Mkutano wa Umoja wa Mataifa

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeandaa kikao cha dharura kuzungumzia majaribio ya makombora ya hivi punde ya Korea Kaskazini baada ya moja ya makombora hayo kuanguka eneo la bahari ya Japan.

Baada ya mkutano huo, balozi wa Marekani Samantha Power alitaka hatua za haraka kuchukuliwa na baraza hilo akitaja majaribio hayo ya makombora kama tishio kwa usalama na amani ya dunia.

Balozi wa Korea Kusini katika Umoja wa Mataifa anasema kuwa Korea Kaskazini inayafanyia makombora majaribio kwa lengo la kuboresha teknolojia yake.