Jeshi la Sudan Kusini laua kikabila,hasa wa Neur

Mofisa wa ngazi ya juu wa umoja wa mataifa kitengo cha haki za binaadamu wamelishutumu jeshi la Sudan Kusini kwa mauaji ya kikabila na ubakaji Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Askari wa Sudan Kusini akiwa kwenye lindo

Mofisa wa ngazi ya juu wa umoja wa mataifa kitengo cha haki za binaadamu wamelishutumu jeshi la Sudan Kusini kwa mauaji ya kikabila na ubakaji yanayoendelea katika kipindi cha mapigano ya hivi karibuni katika mji mkuu wa Juba.

Zeid Ra'ad Al Hussein askari mwaminifu kwa Rais Salva Kiir, kutoka kabila la Dinka, wao wamekuwa wakiwakusudia hasa watu wa kabila la Nuer.Mpinzani mkuu wa Rais Salva Kiir, Riek Machar yeye anatoka katika kabila lengwa la Neur.

Katika baadhi ya matukio, askari wanaarifiwa kwenda nyumba kwa nyumba kuua raia wa kabila la Nuer, matukio hayo hayakuishia hapo, kwani askari hao wameendeleza unyama wao kwa kuwabaka wanawake na wasichana wa kabila hilo la Neur.

Nayo majeshi ya umoja wa mataifa ya kulinda amani yaliyoko nchini Sudan Kusini tayari wameingia lawamani kwa kutowajibika kuwalinda watu wa kabila la Neur na raia kwa ujumla wakati wa vurugu .