Viongozi wakutana kujadili mgogoro wa Sudan Kusini

Rais Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Sudan Kusini salva Kiir Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Sudan Kusini Salva Kiir

Viongozi wa Kikanda kutoka Afrika Mashariki wanakutana katika kikao cha dharura jijini Addis Ababa, Ethiopia kujadili mzozo wa Sudan Kusini.

Marais hao kutoka mataifa wanachama wa IGAD watajadili kwa kina pendekezo la Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa na Muungano wa Afrika AU kutaka kutuma vikosi vya usalama baada ya kuzuka upya kwa mapigano kati ya majeshi ya serikali na vikosi vya aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar.

Hayo yanajiri siku mbili tu baada ya Rais Salva Kiir kuwatimua kazi mawaziri, washauri na wabunge wote wanaoegemea mrengo wa Machar.

Mada zinazohusiana