Homa ya manjano: WHO lawamani CAR

Shirika la afya dunia
Image caption Shirika la afya duniani

Uchunguzi wa shirika la habari la AP umebaini kwamba shirika la afya duniani WHO lilitekeleza makosa makubwa katika kukabiliana na mlipuko wa homa ya manjano Afrika ya Kati.

Uchunguzi huo unasema chanjo milioni moja zilizokuwa zikisafirishwa hadi Angola zilitoweka kutoka kwenye shehena ya chanjo milioni sita za homa hiyo ya manjano.

Baadhi ya chanjo zilipelekwa katika maeneo ambayo hayakuwa yameathiriwa na homa hiyo, huku zilizopelekwa katika maeneo yaliyoathiriwa, zikikosa sindano.

Mada zinazohusiana