Rio2016: Rais wa Brazil asema michezo itafana

Kaimu rais wa Brazil Michel Temer
Image caption Kaimu rais wa Brazil Michel Temer

Kaimu rais wa Brazil Michel Temer, ameelezea matumaini yake kwamba raia wa Brazil watavumbua upya furaha yao ya kiasili wakati michezo ya Olimpiki itakapong'oa nanga siku ya Ijumaa mjini Rio.

Bwana Temer anasema kuwa hatua ya Brazil kuwa mwenyeji wa michezo hiyo, licha ya matatizo ya kisiasa na kiuchumi, kunadhihirisha uwezo wa taifa hilo kujiondoa katika vikwazo vyovyote.

Usalama wa hali ya juu umewekwa mjini Rio kuwazuia waandamanaji dhidi ya kusambaratisha sherehe za ufunguzi.

Gharama ya Sherehe za ufunguzi katika uwanja wa Maracana imepunguzwa, japo waandalizi wameahidi maonyesha ya kufana ya utamaduni wa Brazil.