Michezo ya Olimpiki yafunguliwa rasmi Brazil

Mwanga wa Olimpiki wawashwa Rio De Janeiro
Maelezo ya picha,

Mwanga wa Olimpiki wawashwa Rio De Janeiro

Sherehe za ufunguzi za mashindano ya olimpiki mjini Rio de Janeiro zimefanyika katika uwanaja wa Maracana nchini Brazil.

Tamaduni za Brazil zimesherehekewa ikiwemo densi, muziki na maonyesha ya taa.

Maelezo ya picha,

Rio2016

Wanaridha kutoka zaidi ya nchi 200 wamepita mbele ya umati wa watu.

Waandalizi wanaamini kuwa mashindano hayo yatainua matumaini ya nchi ambayo kwa sasa inakumbwa na hali ngumu ya uchumi na mzozo wa kisiasa.

Maelezo ya picha,

Wanariadha waAfrika Kusini

Hata hivyo waandamanaji kadha wamekuwa wakionyesha hasira zao kutokana gharama kubwa ya kuandaa mashindano hayo.