Trump awaidhinisha mahasimu wake wa Republican

Donald Trump
Maelezo ya picha,

Donald Trump

Mgombea wa urais wa chama cha Republican Donald Trump amechukua hatua ya kuboresha uhusiano na uongozi wa chama cha Republican kwa kumuidhinisha spika wa bunge la waakilishi Paul Ryan.

Mapema wiki hii bwana Trump alikataa kumuidhinisha Ryan anayenuia kuchaguliwa tena

Wakati wa kampeni katika jimbo la Wisconsin bwana Trump alisema kuwa watafanya kazi kwa pamoja hadi wapate ushindi.

Trump pia aliwaidhinisha maseneta wawili wa Republican John McCain na Kelly Ayotte.