Syria wamechukua karibu udhibiti wote wa mji wa Manbij

Polisi wa Syria
Maelezo ya picha,

Polisi wa Syria

Kuna ripoti kuwa wapiganaji wanaoungwa mkono na marekani kaskazini mwa Syria wamechukua karibu udhibiti wote wa mji wa Manbij kutoka kwa Islamic State.

Kikosi cha pamoja cha wakurdi na wapiganaji wa Kiarabu wamekuwa wakipigana kwa majuma kadha kuteka eneo linalotajwa kuwa muhimu karibu na mpaka na Uturuki.

Kikosi hicho kimeingia mjini humo na sasa shirika la haki za binadamu lenye makao yake nchini Uingereza linasema kuwa ni wapiganaji wachache wa IS waliosalia mjini Manbij.

Maelezo ya picha,

Barabara za mji wa Manbij