Tembo aliyekwama kwenye mafuriko kuokolewa Bangladesh

Maofisa wanyamapori wakijaribu kumuokoa tembo huyo aliyenasa
Maelezo ya picha,

Maofisa wanyamapori wakijaribu kumuokoa tembo huyo

Waangalizi wa wanyamapori nchini Bangladesh wamesema wanajaribu kumuokoa Tembo aliyekwama usiku mmoja kwenye mafuriko.

Wakati wa mchana inawawia vigumu kwa sababu ya umati mkubwa wa watu wanaomtazama. Tembo jike huyo aliyefurushwa Bangladesh kutokea nchini India kwenye mafuriko ya mto wiki chache zilizopita.

Tembo huyo amesafiri zaidi ya kilomita mia moja akiwa ndani ya maji huku akiwa amedhoofu.

Maelezo ya picha,

Maelfu ya wanyamapori huama katika eneo hilo wakati wa mafuriko

Mtaalamu wa wanyamapori Asim Mallik aliiambia BBC kuwa timu yake itajaribu kumtafuta tembo huyo nchi kavu wakati wa usiku ambapo hakutakuwa na umati wa watu, kabla ya hawajatulia na kumwokoa.