Upinzani wataka Rais kung'oka Venezuela

Kiongozi wa upinzani Henrique Capriles amesema tume ya uchaguzi inafanya vichekesho kwa kuchelewesha kura za maoni Haki miliki ya picha EPA
Image caption Kiongozi wa upinzani Henrique Capriles amesema tume ya uchaguzi inafanya vichekesho kwa kuchelewesha kura za maoni

Wapinzani nchini Venezuela wamekasirishwa na viongozi wa tume ya Uchaguzi wakati wa kukusanya kura za maoni za kumwondoa madarakani Rais Nicolas Maduro.

Tume hiyo imesema kuwa itafanyika mwishoni mwa mwezi wa oktoba.

Wapinzani wamesema kuwa ni muhimu kufanya hivyo na ikishindikana Maduro anaweza kuharibu uchaguzi wa Urais.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Tibisay Lucena kiongozi wa tume ya uchaguzi amesema kura hiyo itafanyika mwishoni mwa mwezi wa oktoba.

Lakini kama ni mwakani Makamu wake atashikilia nafasi yake na kuruhusu chama chake cha kijamaa kuendelea kubaki madarakani.

Gavana wa jimbo la Miranda Henrique Capriles, ameeleza kucheleweshwa huko kuwa ni ujinga na kuhimiza maandamano ya wapinzani kuendelea septemba.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Nicolas Maduro

Nchi ya Venezuela inakumbana na matatizo ya kiuchumi ambapo upinzani wanamlaumu Rais Maduro kuwa sababu kuu.