Afungwa miaka 5 jela kwa kumtesa mbwa Marekani

Mbwa huyo Caitlyin, alipoteza sehemu ya ulimi wake na alifanyiwa upasuaji kadhaa baada ya kufika kwenye kituo cha kuwanusuru wanyama eneo la Charleston

Chanzo cha picha, Facebook/Charleston Animal Society

Maelezo ya picha,

Caitlyin

Mwanamume mmoja nchini Marekani amekiri kosa la kuufunga mdomo wa mbwa mwaka jana America

Vyombo vya habari katika jimbo la South Carolina vimeripoti kuwa William Dodson, mwenye umri wa miaka 42, anakabiliwa na kifungo cha miaka mitano jela.

Hukumu yake imeahirishwa hadi pale ripoti itakapokuwa tayari .

Mbwa huyo Caitlyin, alipoteza sehemu ya ulimi wake na alifanyiwa upasuaji kadhaa baada ya kufika kwenye kituo cha kuwanusuru wanyama eneo la Charleston huku mdomo wake ukiwa umefungwa mwezi mei mwaka jana.

Catylin alinunuliwa kwa dola 20

Kwa sasa ana umri wa miaka miwili na anaishi na familia mpya , lakini bado hushtuka shtuka na ana mfadhaiko.

Mbali na kutumiakia kifungo, William Dodson anakabiliwa na adhabu ya kulipa faini ya $5,000 .

Chanzo cha picha, Facebook/Carleton animal society

Maelezo ya picha,

Caitlyn

Amekua katika jela ya kaunti ya Charleston County tangu tarehe 1 Juni mwaka jana.

Akwa mujibu wa polisi, William Dodson alimnunua Caitlyn, na kumuita jina Diamond, kwa dola $20

Alisema alifunga mdomo wake kwa waya wa umeme kwasababu anabweka kupita kiasi, lakini mbwa aliweza kukata mnyororo na kutoroka.

Dodson Pia anakabiliwa na kifungo cha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumiliki silaha aina ya pisto kinyume cha sheria.

Chanzo cha picha, Facebook/Carleton animal society

Maelezo ya picha,

Caitlyn

Kwenye ukurasa wake wa Facebook, shirika la wanyama la Charleston limeweka picha ya kuonyesha uungaji mkono wa kesi hiyo.

Wamekua wakituma picha za matukio kuhusu mbwa huyo tangu kesi ilipoanza , ambayo imevutia hisia kimataifa.

Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Joe Elmore. Amesema : " kipaumbele chetu cha kwanza ni afya ya Caitlyn na tunazingatia mahitaji yake ya kipekee kwa ajili ya kuboresha maisha yake na tutaendelea kufanya hivyo."