Akamatwa kwa kupanda mnara wa makao makuu ya Trump Marekani

Polisi wakijitahidi kumuondoa
Image caption Polisi wakijitahidi kumuondoa

Mtu mmoja aliyejaribu kupanda jengo la Trump Tower lililopo jijini New York, ameondolewa na polisi katika jengo hilo baada ya kuchomwa na vioo vya jengo hilo lenye ghorofa 58 ambalo ni makao makuu ya kampeni za kumchagua Donald Trump.

Image caption Mpandaji alionekana amelewa

Trump anaishi kwenye chumba cha juu ya ghorofa hilo lakini kwa sasa anafanya kampeni zake nje ya mji.

Mpandaji alijivuta huku akiwa akionekana kuwa amelewa, akitaka kuingia ndani ya jengo hilo.

Image caption Umati wa watu ukishuhudia polisi wakimuondoa

Polisi waliofika eneo la tukio wamesema hawakuweza kutambua nini haswa lilikuwa lengo lake.

Image caption Hatimaye polisi walifanikiwa kumuingiza ndani ya jengo hilo