Ashley Williams ajiunga na Everton ya ligi kuu England

Ni mchezaji wa tatu kununuliwa na meneja Koeman
Maelezo ya picha,

Ni mchezaji wa tatu kununuliwa na meneja Koeman

Timu ya Everton imemsainisha kapteni wa Wales, Ashley Williams kutoka kwa wapinzani wao wa ligi kuu Swansea kwa gharama inayokadiliwa kufikia Euro milioni 12.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 31, ni mchezaji wa tatu kununuliwa na meneja Ronald Koeman baada ya kiungo wa Senegal Idrissa Gueye na mlinda mlango Maarten Stekelenburg.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Amedumu Swansea kwa miaka nane

Wapo pia kwenye maongezi kumsainisha kiungo wa Crystal Palace Yannick Bolasie na wa beki wa Sunderland Lamine Kone.