Olimpiki: Rangi ya maji ya kuogelea kurejea kawaida baada ya kuwa ya kijani

Maji ya bwawa hilo yalibadilika rangi kutokana na kuzidi kwa kiwango cha Alkalini
Image caption Maji ya kidimbwi hicho yalibadilika rangi kutokana na kuzidi kwa kiwango cha Alkalini

Waandaaji wa michuano ya Rio wamesema kuwa Bwawa la kuogelea litarudi kwenye rangi yake ya awali baadaye hii leo, baada ya kubadilika na kuwa na rangi ya kijani siku ya jana wakati michuano hiyo ikiendelea.

Kwa mujibu taarifa ya yake maji ya bwawa hilo yalibadilika rangi kutokana na kuzidi kwa kiwango cha Alkalini.

Amesema kuwa wapimaji wa maji hawakujali wingi wa waogeleaji kama wataathiriwa na kiwango cha PH, na Chlorine.

Image caption Wapimaji wa maji hawakujali wingi wa waogeleaji kama wataathiriwa na kiwango cha PH na Chlorine

Washindanaji walisema ilikuwa vigumu kuwaona wenzao kwenye maji ya kijani.

Waandaaji wa Michuano ya Rio wamesema maji hayo hayana athari yoyote kiafya.