Ugonjwa wa polio bado tishio nchini Nigeria

Ni kesi ya kuripotiwa tokea mwaka 2014
Image caption Ni kesi ya kuripotiwa tokea mwaka 2014

Nigeria imeripoti kesi mbili za ugonjwa wa polio katika jimbo la Borno eneo ambalo kuna idadi kubwa ya wapiganaji wa Boko Haram.Watoto wawili wamepooza kutokana na ugonjwa huo.

Shirika la afya duniani limesema ndio kesi za kwanza kwa miaka miwili sasa.

Image caption Chanjo ya polio hutolewa kote barani Afrika

Kesi hizi zimekwamisha matumaini ya kukomesha Polio kwa mwaka huu.

Umoja wa mataifa umekanusha uvumi kuwa chanjo za polio zina lengo la kusababisha kutozaa kwa wailsamu