Arsenal kuchuana na Liverpool EPL

Kocha Jurgen Klopp wa Liverpool na mwenziwe Atsene Wenger wa Arsenal kulia
Maelezo ya picha,

Kocha Jurgen Klopp wa Liverpool na mwenziwe Atsene Wenger wa Arsenal kulia

Mchezaji mpya aliyesajiliwa hivi karibuni Granit Xhaka na Rob Holding wanatarajiwa kuichezea Arsenal kwa mara ya kwanza dhidi ya Liverpool lakini mabeki Mertesacker ,Gabriel na Carl Jenkison wote wakiwa na majeraha.

Danny Welbeck pia anauguza jeraha,huku wachezaji fainali ya Euro2016 wakiwa Laurent Koscielny na mwenzake Giroud bado wakiwa hawako tayari kushiriki katika mechi hiyo.

Liverpool itamkosa mshambuliaji wake mahiri Daniel Sturridge na James Milner kutokana na majeraha ya nyonga na kisigino.

Hatahivyo huenda Sadio Mane ,Georginio Wijnaldum na Joel Matip wakaanzishwa kwa mara ya kwanza.