Bournemouth kuikabili Manchester United

Mourinho na Wayne Rooney

Chanzo cha picha, Ben Hoskins

Maelezo ya picha,

Mourinho na Wayne Rooney

Mchezaji aliyesajiliwa kwa kiasi kikubwa duniani Paul Pogba hatoanza katika mechi dhidi ya Bournemouth.

Hii ni kwa sababu anahudumia marufuku ya mechi moja baada ya kupewa kadi mbili za manjano akiichezea Juventus nchini Italy.

Chris Smalling pia hatoshiriki mechi hiyo lakini wachezaji wapya Zlatan Ibrahimovic,Henrikh Mkhitaryan na Eric Bailly watashiriki.

Winga wa klabu ya Bournemouth Junior Stanislas yuko nje na jeraha la ngiri lakini Jordon Ibe aliyesajiliwa kutoka Liverpool kwa kitita cha pauni milioni 15 ni miongoni ya watakaoshiriki mechi hiyo.