Elaine Thompson ashinda mbio za mita 100 za wanawake

Bingwa wa mbio za mita 100 Elaine Thompson
Image caption Bingwa wa mbio za mita 100 Elaine Thompson

Mwanariadha wa Jamaica Elaine Thmpson ndio mshindi wa medali ya dhahabu upande wa wanawake katika michezo ya Olimpiki mjini Rio de Janeiro.

Thompson mwenye umri wa miaka 24 alishinda mbio hizo katika mda wa sekunde 10 nukta 71.

Bingwa wa mbio hizo naye pia kutoka Jamaica, Fraser Pryce mwenye umri wa miaka 29 ambaye alikuwa anajaribu kuwa mwanamke wa kwanza kushinda mbio hizo mara tatu mfululizo ,alimaliza wa tatu.

Mwanariadha wa Marekani Tori Bowie alishinda medali ya shaba.

Mwanariadha wa Uholanzi Dafne Schippers aliyemaliza wa pili nyuma ya Fraser-Pryce katika michezo ya dunia ya mwaka 2015 alimaliza wa tano.

''Nilifika katika utepe na kuona kwamba niko mbele ya kila mtu nilishindwa namna ya kusherehekea''alisema Thomspon.

Mada zinazohusiana