Kenya yashinda dhahabu yake ya kwanza Rio de Janeiro

Jemima Sumgong

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Jemima Sumgong

Jemima Jelagat Sumgong ameishindia Kenya medali yake ya kwanza katika mbio za marathon upande wa wanawake.

Sumgonda alishinda katika mda wa saa 2 dakika 24 na sekunde nne mbele ya mzaliwa mwengine wa Kenya ambaye amechukua uraia wake Bharian Eunice Kirwa.

Bingwa wa dunia Mare Dibaba wa Ethiopia alikuwa wa tatu.

Kenya sasa ina mdeali moja ya dhahabu na mbili za fedha baada Vivian Cheruiyot kushinda fedha katika mbio za mita 10,000 upande wa wanawake naye Tanui akaishindia fedha katika mbio hizo upande wa wanaume.