Mourinho aanza na ushindi dhidi ya Bournemouth

mourinho
Image caption mourinho

Mkufunzi Jose Mourinho alianza vyema harakati zake za kushinda kombe la ligi ya Uingereza msimu huu baada ya kuishinda Bournemouth.

Juan Mata,ambaye alitolewa baada ya kuanza katika kombe la Community Shield alianza kufunga baada ya mchezaji wa Bournemouth Simon Francis kufanya masikhara.

Wayne Rooney alifunga bao la pili kwa kichwa kabla ya Zlatan Ibrahimovic kupata bao lake la kwanza akiwa na Manchester United kupitia mkwaju wa yadi 25.

Adam Smith aliifungia timu hiyo ya nyumbani bao la kufutia machozi.

United walicheza mechi hiyo bila Paul Pogba,huku kiungo wa kati Henrikh Mkhitaryan akicheza kama mchezaji wa ziada baada ya Mata kuanzishwa.

Mada zinazohusiana