Barcelona yaichapa Sevilla kwa mabao 2-0

Messi na Suarez

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Messi na Suarez wakishangilia goli

Miamba ya soka ya Hispania Barcelona wametwaa ubingwa wa Super Cup kwa kuifunga klabu ya Sevilla kwa mabao 2-0.

Mabao ya Barcelona yalifungwa na mshambuliaji Luis Suarez na Munir El Haddadi magoli yote yakifungwa katika kipindi cha pili cha mchezo.

Licha ya Barca kushinda mchezo huo uliochezwa katika dimba la Sanchez Pizjuan kocha wa kikosi Luis Enrique, alilazimika kufanya mabadiliko kwa beki wake Jeremy Mathieu na kiungo mkongwe Andres Iniesta waliopata majeruhi katika mchezo huo.

Kukosekana kwa mashambuliaji Neymer anayeitumikia timu ya taifa ya Brazil katika michezo ya Olimpic kuliwafanya Barcelona kumtumia Arda Turan kama mshambuliaji wa tatu nyuma ya Messi na Suarez.