Nyumba ya muuaji wa msichana wa Kiisraeli yabomolewa

Nyumba ya msichana wa Kiisraeli aliyeuawa na mwanamume wa Kipalestina Haki miliki ya picha AFP
Image caption Nyumba ya msichana wa Kiisraeli aliyeuawa na mwanamume wa Kipalestina

Jeshi la Israel linasema kuwa limeharibu nyumba ya raia wa Kipalestina aliyemdunga kisu na kumuua msichana wa Iiisraeli chumbani mwake.

Jeshi hilo limesema kuwa Mohammed Nasser Tarayrah alivunja na kuingia katika nyumba iliopo katika makaazi ya Kiryat Arba mnamo mwezi Juni na kumshambulia msichana huyo mwenye umri wa miaka 13 Hallel Yaff Ariel alipokuwa akilala kabla ya kuuawa na mlinzi wa makaazi hayo.

Sera ya Israel ya kuziharibu nyumba za raia wa Palestina wanaofanya mashambulio imekosolewa na wengi kama adhabu ya jumla.

Serikali ya Israel inasema kuwa hatua hiyo inawazuia wengine ambao wangependelea kutekeleza kitendo kama hicho.

Mada zinazohusiana