Ahmad Salkida ahusishwa Boko Haram, Nigeria

Nigeria
Image caption Ahmad Salkida

Mwandishi mmoja wa habari nchini Naijeria, anasakwa na mamlaka za juu za jeshi la nchi hiyo kwa madai kwamba ana uhusiano wa moja kwa moja na wanamgambo wa Boko Haram, ingawa yeye mwenyewe amekanusha kuliunga mkono kundi hilo.

mwandishi wa habari huyu ambaye makao yake makuu ni Dubai ,Ahmad Salkida, amesema kwamba yuko tayari kufanya safari kuelekea nchini Nigeria kuhojiwa na jeshi la nchi hiyo.

Jeshi la Nigeria limetoa waraka unaomhusu Salkida baada ya kuweka kiungo cha habari kwenye mitandao wa kijamii kuhusian na video ya kundi la Boko Haram inayoonesha baadhi ya wasichana ambao walitekwa na kundi hilo katika mji wa Chibok Kaskazini mwa nchi hiyo miaka miwili iliyopita .

Jeshi hilo limesema kwama wanaamini kwamba mwandishi huyo ana taarifa za wapi wanashikiliwa wasichana hao.

Awali Ahmad Salkida, aliwahi kufanya mahojiano na kiongozi wa kundi la Boko Haram na inasemekana aliwahi kuhusika katika jaribio la upatanishi lililoshindwa baina ya serikali ya rais wa zamani Goodluck Jonathan na kundi hilo la Boko Haram.