Edgar Lungu ashinda uchaguzi wa urais Zambia

Rais Edgar Lungu wa Zambia
Maelezo ya picha,

Rais Edgar Lungu wa Zambia

Rais wa Zambia Edgar Lungu ametangazwa mshindi wa matokeo ya uchaguzi wa urais kulingana na matokeo rasmi ya uchaguzi.

Tume ya uchaguzi nchini Zambia imesema kuwa Lungu alijipatia asilimia 50.35 siku ya Alhamisi ,ikiwa imepita asilimia 50 inayohitajika ya kuzuia raundi ya pili kulingana na sheria mpya ya uchaguzi.

Mpinzani wake Hakainde Hichilemi alijipatia asilimia 47.67 ya kura.

Awali,chama chake cha UNPD kilijiondoa katika shughuli ya kuhakiki kura akidai kuwa kulikuwa na udanganyifu.