Waandishi walio na uhusiano na Boko Haram wasakwa Nigeria

Boko Haram
Image caption Boko Haram

Jeshi la Nigeria sasa linataka kumhoji mwandishi mmoja kuhusiana na uhusiano wake na kundi la Boko Haram.

Hatua hiyo inajiri baada ya kanda ya video inayowaonyesha wasichana waliotekwa nyara katika mji wa kaskazini mashariki wa Chibok.

Taarifa ya jeshi imemtaja Ahmed Salkida na inasema ana habari kuhusu hali na eneo walikofichwa wasichana hao.

Pia linataka kuzungumza na Ahmed Bolori na Aisha Wakil.

Taarifa hiyo inaongeza kwamba hakuna wasiwasi watu hao wana uhusiano wa karibu na kundo la Boko Haram mbali na mawasiliano.

Bwana Salkida anaishi Dubai na anaaminika kuwa mtu aliyechapisha kanda za video za Boko Haram-ijapokuwa hajatoa tamko lolote.

Katika mahojiano na BBC bwana Bolari amesema aligundua kwamba alikuwa akitafutwa katika mitandao ya kijamii na kwamba tayari alikuwa amewasiliana na jeshi.

Amekana madai hayo.Bwana Wakil hajatoa tamko lolote.

Mada zinazohusiana