Upinzani Zambia:Rais Lungu anapendelewa

Rais wa Zambia,Edgar Lungu

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Rais wa Zambia,Edgar Lungu

Upinzani nchini Zambia umeshutumu mamlaka ya uchaguzi kwa mipango ya kumpendelea Rais Edgar Lungu na kusema watapinga matokeo hayo katika Mahakama ya Katiba.

Siku ya Jumatatu Rais wa Zambia, Edger Lungu, alitangazwa kuwa mshindi licha ya malalamiko ya kutoka Chama cha upinzani kuhusu udanganyifu na wizi wa kura. Tume ya uchaguzi imesema amepata zaidi ya ya asilimia hamsini ya kura akimshinda mpinzani wake mkuu, Hakainde Hichilema, ambaye alipata asilimia arobaini na nane ya kura zote.

Rais wa chama cha Movement for Multiparty Democracy, Dk Nevers Mumba, amesema analo mkononi pingamizi la kuzuia matokeo yasitangazwe, jambo ambalo lilipuuzwa na tume.

"tulienda mahakamani Jumapili na tukapewa pingamizi la kuzuia tume ya uchaguzi isiendelee kutangaza matokeo ya uchaguzi na wakapuuza agizo la mahakama na kuendelea kutangaza kura zenye mgogoro ambazo zinatonyesha kuwa wanaongoza dhidi yetu, kwasababu tumekuwa tukiongoza muda wote, kama kusingekuwa na wizi wa kura''

Amesema chama chake kimewakamata watu tofauti wakichezea karatasi za kupigia kura na kwa sababu hiyo hivi sasa wapo chini ya ulinzi.