Aliyekuwa Rais wa Zanzibar amezikwa
Huwezi kusikiliza tena

Aliyekuwa Rais wa Zanzibar azikwa

Aliyekuwa Rais wa Zanzibar Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi amezikwa leo nyumbani kwake Migombani Zanzibar. Mzee Jumbe alikuwa Rais kwa kipindi cha miaka 12 tangu 1972 hadi 1984. Pamoja na mambo mengine mengi, atakumbukwa kwa mabadiliko aliyoyafanya ya muundo wa serikali na katiba vilivyoweka msingi wa aina ya muundo wa serikali iliyopo hivi sasa. Mwandishi wetu Sammy Awami alihudhuria mazishi hayo na kutuandalia taarifa ifuatayo.