Donald Trump aibadilisha timu yake ya kampeni

Donald Trump
Image caption Donald Trump

Mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican Donald Trump ameifanyia mabadiliko timu yake ya kampeni kwa mara ya pili katika kipindi cha miezi miwili akiteua meneja mpya na afisa mkuu.

Pollster Kellyanne Conway ndio meneja mpya huku Stephen Bannon wa kituo cha habari cha Breitbart akiwa afisa mkuu.

Paul Manarfort anasalia mwenye kiti wa kampeni yake.Bwana Trump amekiambia chombo cha habari cha AP kwamba viongozi hao wapya ni wachapakazi.

Umaarufu wa Bw Trump umeonekana ukishuka tangu mkutano wa chama hicho uliofanyika mwezi uliopita.

Anamfuata mpizani wake wa Democrat Hillary Clinton katika umaarufu wa kitaifa pamoja na majimbo muhimu yalio na ushindani mkali.

Mada zinazohusiana