Matusi yamfanya Justin Bieber kufunga akaunti yake ya Instagram

Justin Bieber
Maelezo ya picha,

Justin Bieber

Justin Bieber ameifunga mbali akaunti yake ya mtandao wa instagram baada ya mashabiki kadhaa kumtusi mpenziwe.

Msanii huyo wa Canada na mpenziwe wa zamani walikuwa wakishtumiana katika mtandao huo wa picha na video.

Tatizo hilo lilianza baada ya Justin Bieber kuchapisha picha kadhaa za yeye na mpenzi wake mpya Sofia Richie.

Baada ya kupokea matusi kutoka kwa mashabiki wake alionya kuibinfasisha akaunti yake iwapo vijana wanaomtusi hawatasita kumtusi.

''Iwapo nyinyi ni mashabiki wa ukweli musingewachukia watu ninaowapenda''.

Inaonekana Bieber alifuta mtandao wake wa Istagram kwani unapofungua unapata maneno yanayokwambia ''pole mtandao huu hautumiki''.

Selena Gomez alichapisha tamko lake chini ya picha hiyo akisema iwapo hutaki kushambuliwa koma kuweka picha ya mrembo wako.

Selena Gomez

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Selena Gomez

Alindika:''Iwapo huwezi kuvumilia matamshi ya chuki kutoka kwa mashabiki ni muhimu iwe kati yenu tu''.

''Usiwakasirikie mashabiki wako,wanakupenda na walikushabikia kabla ya mtu yeyote kufanya hivyo''.

Lakini baada ya matamshi hayo ya Selena ,Justin alijibu akidai katika ujumbe uliomaanisha kwamba msanii huyo alimtumia ili kupata umaarufu.

''Inachekesha kuona kwamba watu walionitumia kujipatia umaarufu sasa wananishtumu''.