Kenya yashindwa kufuzu fainali ya mita 5000 Rio de Janeiro

Wanariadha wa Kenya Haki miliki ya picha Alamy
Image caption Wanariadha wa Kenya

Kenya kwa mara ya kwanza imeshindwa kufuzu katika fainali ya mbio za mita 5000 upande wa wanaume katika michezo ya Olimpiki ya Rio de Janeiro.

Hii ni baada ya wanariadha Caleb Ndiku na Kiplangat Koiech kushindwa kufuzu katika makundi yao.

Hatahivyo kenya itawakilishwa na mwanariadha kutoka kenya anayekimbilia marekani Bernard Lagat.

Fainali ya mbio hizo itafanyika siku ya Jumamosi

Mada zinazohusiana