Wana miereka wapigwa marufuku na WWE

Alberto Del Rion na Paige
Maelezo ya picha,

Alberto Del Rion na Paige

Wana miereka Alberto Del Rio na mwenzake Paige wamepigwa marufuku kwa mda kwa kukiuka sera za shirika la wana miereka la WWE.

Shirika la WWE halijatoa maelezo kuhusu marufuku hiyo lakini sera ya shirika hilo inasisitiza kuhusu umuhimu wa kutohusisha mchezo huo na mihadarati.

Ni mara ya kwanza kwa wana miereka hao maarufu kukiuka sheria za WWE.

Wote wawili wamesimamishwa kwa mda wa siku 30 na watakosa mashindano ya wikendi ya Brooklyn ,huko New York.

Kati yao hakuna aliyezungumza kuhusu marufuku hiyo ambayo ilitolewa siku ya kuzaliwa kwa Paige.

Baadhi ya mashabiki wameonyesha kuhuzunishwa na marufuku hiyo.

Lakini wengine wanasema kuwa marufuku hiyo ni njama ya kupunguza umaarufu wa wana miereka hao.