Santos achaguliwa tena kuongoza chama tawala Angola

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jose Eduardo dos Santos amekuwa madarakani kwa miaka 36

Rais wa Angola, Jose Eduardo dos Santos aliyeongoza kwa miaka 36 amechaguliwa tena kuwa kiongozi wa chama tawala cha MPLA.

Uchaguzi wa bunge unatarajiwa kufanywa mwaka ujao, na kiongozi wa chama kinachoshinda ndiye anayekuwa rais.

Rais dos Santos alisema awali mwaka huu, kwamba ataondoka madarakani mwaka wa 2018, lakini ameshawahi kutoa ahadi kama hizo kabla.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 73, analaumiwa kuwa amekusanya madaraka mengi na mali, kwenye mikono ya familia yake na washirika wake wakubwa kisiasa.